• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HONGERA MANISPAA YA SONGEA KWA KUPATA HATI SAFI. "RC RUVUMA APONGEZA"

Tarehe ya kuwekwa: June 18th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali “Balozi” Wilbert Ibuge amewapongeza Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Songea kwa kukusanya mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 99.01%.

Hayo yamebainishwa katika kikao cha baraza Maalum la Madiwani  kilichofanyika leo 18 Juni 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kupitia taarifa za Mkaguzi Mkuu wa ndani  wa hesabu za Serikali (CAG)  kwa mwaka wa fedha 2019/2020,  kikao kilichohudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani wa kata zote 21 zilizopo katika Manispaa ya Songea, wakuu wa Idara na viongozi mbalimbali.

Akitoa pongezi hizo Ibuge amesema,   Halimashauri ya Manispaa ya Songea katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 imekusanya  kiasi  cha Tshs. 3,374,756,150.90/= kati ya kiasi kilichotarajiwa kukusanywa ambacho ni Tshs. 3,408,416,455/=  nakufikia lengo kwa asilimia 99.01%.

Alibainisha kuwa,  Halmashauri ya Manispaa ya Songea  imechangia Tshs. 286,304,029/= ambayo ni sawa na asilimia 98.17%  kwa ajili ya kuwezesha  mfuko wa wanawake 4%, vijana 4%  na watu wenye ulemavu 2%,  fedha ambayo  imesaidia kutoa fursa  kwa vijana kujiajiri  wenyewe pamoja  na kuleta  maendeleo kwa jamii.

Alisema  “ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi Mkuu Mkazi  wa hesabu za Serikali  umetekelezwa vizuri  na kufanikisha kujibu hoja zilizotolewa kwa zaidi ya asilimia 95% kati ya hoja zilizotolewa na kupelekea Halmashauri  ya Manispaa Songea kupata hati safi. Pia   Amewataka viongozi  hao  kuhakikisha wanamaliza kujibu hoja zote ambazo  bado hazijakamilika kufungwa  hadi kufikia tarehe 30 Septemba ziwe zimejibiwa. “ Aliwapongeza.”

 Ametoa  Rai kwa Waheshimiwa Madiwani na wataalamu  kushiriki ipasavyo kujibu hoja zote pamoja na kutekeleza maelekezo wanayopewa kutoka kwa Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali wa ndani na kutoruhusu marudio ya hoja zilezile ambazo hujitokeza kila mwaka.  “Ibuge Alieleza”

Aidha amewataka Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanatekeleza ahadi walizoahidi kwa wananchi katika kipindi cha kampeni  na kusimamia vizuri miradi mikubwa iliyokamilika  ikiwemo na stendi ya Tanga na machinjio  ya kisasa ambayo imeanza kutumika ambapo inasaidia kuongeza mapato na kuleta maendeleo katika Halmashauri  na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Ibuge ameziagiza Halmashauri zote  Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanalipa madeni yote  ya wazabuni kwa wakati,  kuendesha  vikao vya ukaguzi vya mapato  ya ndani  mara kwa mara kwa mujibu wa sheria. Wakurugenzi wote kila Halmashauri husika  watahakikisha  wanashiriki vikao vya ukaguzi pamoja na Waheshimiwa Madiwani ili kuleta ushirikiano wa pamoja  na kutatua changamoto za Halmashauri husika.’Alisisitiza’

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano amesema kuwa Baraza la Madiwani limejipanga kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Serikali katika kuhakikisha wanaleta maendeleo katika Manispaa ya Songea.

IMEANDALIWA NA,

AMINA PILLY,

AFISA HABARI MANISPAA,

18.06.2021.

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa