HALMASHAURI ya Manispaa Songea mkoani Ruvuma ina jumla ya viwanda 512 kati ya viwanda hivyo kiwanda kikubwa ni kimoja ambacho ni cha kusindika tumbaku kinachomilikiwa na chama cha ushirika cha SONAMCU ambacho kwa sasa hakifanyi kazi.Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo anavitaja Viwanda vya kati katika Manispaa hiyo kuwa vipo tisa, viwanda vidogo ni 132 na viwanda vidogo sana ni viwanda 371.
Hata hivyo anasema viwanda hivyo vya kati,vidogo na vidogo sana ni vya kukamua mafuta ya alizeti, usindikaji wa Mihogo, usindikaji wa mboga mboga na Matunda, kukoboa Mpunga na viwanda vya kukoboa na kusaga nafaka.Anayataja matarajia ya baadaye ya Manispaa hiyo kuwa ni halmashauri inaandaa mradi wa kimkakati ili kujenga soko la kisasa la Manzese ambalo litaboresha huduma kwa wananchi pamoja na kuiletea mapato Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Anasema Manispaa hiyo inatekeleza miradi mikubwa ambapo Serikali imetoa fedha kupitia programu ya uimarishaji na uendelezaji wa miji (ULGSP) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya miundombinu.Anaitaja miradi hiyo kuwa ni Ujenzi wa machinjio hii unafanyika katika Mtaa wa Tanga, kata ya Tanga, mradi huu ulianza mwezi Julai, 2017 na ulitarajiwa kukamilika Oktoba, 2018.
Anazitaja gharama ya mradi huu kuwa zaidi ya bilioni 3.2 na kwamba Kukamilika kwa mradi huu kutaboresha uchinjaji wa wa kisasa hivyo kuongeza ubora wa bidhaa za nyama. Mradi huu unajengwa chini ya programu ya uboreshaji wa miji na Manispaa (ULGSP).
Mradi wa pili anautaja kuwa ni ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi unafanyika katika Mtaa wa Tanga, kata ya Tanga, mradi huu ulianza mwezi machi 2018 na unategemea kukamilika mwezi septemba, 2019.
Anasema mradi huo unagharimu Gharama shilingi bilioni . 6,189,340,930.00 Kukamilika kwa mradi huu utaboresha sekta ya usafirishaji na kupunguza msongamano kati kati ya mji hivyo kuruhusu kituo cha mabasi kinachotumika sasa kutumika kwa mabasi yaendayo wilayani na maeneo yanayoizunguka Manispaa ya Songea “Mradi huu unajengwa chini ya programu ya uboreshaji wa miji na Manispaa (ULGSP). Mradi huu unajengwa chini ya programu ya uboreshaji wa miji na Manispaa (ULGSP)’’,anasisitiza Sekambo.
Akizungumzia mradi wa ujenzi wa barabara katika kiwango cha lami manispaa ya Songea,Sekambo anasema,Ujenzi wa barabara kiwango cha lami km 10.3 katika barabara za kati kati ya Mji umeanza mwezi Machi, 2018 na unategemea kukamilika mwezi Septemba, 2019.
Anamtaja Mkandarasi aliyefuzu kujenga barabara hizo kuwa ni Kampuni ya SIETCO ya watu wa Jamhuri ya China na kwamba hadi kukamilika mradi huo utagharimu jumla ya Tshs. 10,960,078,230.00.Amesema Kukamilika kwa mardi huu kutaboresha mwonekano wa mji wa Songea na kwamba mradi huu unajengwa chini ya programu ya uboreshaji wa miji na manispaa (ULGSP).
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa