SERIKALI imetoa fedha kupitia programu ya uimarishaji na uendelezaji wa miji (ULGSP) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya miundombinu kama ifuatavyo
Ujenzi wa machinjio ya kisasa: Ujenzi wa machinjio hii unafanyika katika Mtaa wa Tanga, kata ya Tanga, mradi huu ulianza mwezi Julai, 2017 na unategemea kukamilika mwezi Juni, 2018. Gharama ya mradi huu ni Tshs. 3,216,237,382.40. Kukamilika kwa mradi huu utaboresha uchinjaji wa wa kisasa hivyo kuongeza ubora wa bidhaa za nyama. Mradi huu unajengwa chini ya programu ya uboreshaji wa miji na Manispaa (ULGSP).
Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Mkoa.ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi unafanyika katika Mtaa wa Tanga, kata ya Tanga, mradi huu ulianza mwezi machi 2018 na unategemea kukamilika mwezi septemba, 2019. Gharama ya mradi huu ni Tshs. 6,189,340,930.00 Kukamilika kwa mradi huu utaboresha sekta ya usafirishaji na kupunguza msongamano kati kati ya mji hivyo kuruhusu kituo cha mabasi kinachotumika sasa kutumika kwa mabasi yaendayo wilayani na maeneo yanayoizunguka Manispaa ya Songea na hivyo kuongeza mapato ya ndani. Mradi huu unajengwa chini ya programu ya uboreshaji wa miji na Manispaa (ULGSP). Mradi huu unajengwa chini ya programu ya uboreshaji wa miji na Manispaa (ULGSP).
Ujenzi wa barabara km 10.3 kiwango cha lami kwa barabara za mitaa. Ujenzi wa barabara kiwango cha lami km 10.3 katika barabara za kati kati ya Mji umeanza mwezi Machi, 2018 na unategemea kukamilika mwezi Septemba, 2019. Mkandarasi aliyefuzu kujenga barabara hizo ni SIETCO. Hadi kukamilika mradi huo utagharimu jumla ya Tshs. 10,960,078,230.00 Kukamilika kwa mardi huu utaboresha mwonekano wa mji. Mradi huu unajengwa chini ya programu ya uboreshaji wa miji na manispaa (ULGSP).
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 17,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa