MJI wa Songea ulianzishwa mwaka 1897 kama Kituo cha Kijeshi cha Kijerumani,mji huo ulikuwa Makao makuu ya utawala wa wakoloni wa kijerumani na wilaya ya Songea.Tangu wakati wa utawala wa kikoloni hadi sasa Mji wa Songea umeendelea kuwa makao makuu ya mkoa wa Ruvuma.Mji wa Songea una umaarufu wa mashujaaa waliopigana vita vya Majimaji kati ya mwaka 1905 hadi 1907 ambapo mashujaa 67 walinyongwa mwaka 1906 na kuzikwa katika kaburi moja ambapo Nduna Songea Mbano kutokana na umaarufu wake ,alinyoingwa na kuzikwa katika kaburi la pekee yake.Mji wa Songea ulizinduliwa rasmi kuwa mji wa kihistoria,kishujaa na kiutalii mwaka 2010.Mji huo ni miongoni mwa miji michache nchini yenye hazina kubwa ya utajiri wa historia ya utajiri katika nchi yetu.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai 30,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa