WATU wanaodaiwa kuwa ni Mganga na Mchungaji feki wamekamatwa na Jeshi la polisi Mkoani Ruvuma wakijaribu kuwatapeli wananchi kwa lengo la kujipatia fedha .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma ACP Simon Maigwa, amemtaja mtuhumiwa Deo Mapunda miaka 32 kabila la mmatengo ambaye amejifanya mganga wa kienyeji na kudai kuwa anaweza kufufua watu waliokufa akishirikiana na wenzake wawili wakiwa na jeneza ambalo ndani yake kulikuwa na mtuhumiwa Abdul.
Maigwa alifafanua kuwa mtuhumiwa huyo aliwadanganya wanakijiji kuwa marehemu huyo angefufuka baada ya masaa sita baada ya kitendo wananchi walieanda nyuma ya nyumba hiyo na kugundua kuwa mtu huyo ametoweka katika mazingira ya kutatanisha ndipo wananchi waligundua kuwa wanataka kutapeliwa .
“wananchi hao waliamua kumkamata na kuchoma moto jeneza hilo kisha kumfikisha mtuhumiwa kituo cha polisi Songea, katika mahojiano hayo mganga huyo alikiri kuwa yeye sio mganga anayeweza kufufua mtu ila ni njia aliyoweza kuitumia kwa ajili ya udanganyifu”.amesema Maigwa.
Kamanda ameendelea kuelezea kuwa katika nyumba ya wageni ya maeneo ya Bombambili Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ndipo alipokamatwa mtuhumiwa Adinikas Kyuvu miaka 45 raia wa Kenya aliyejifanya mchungaji kwa lengo la kuwatapeli wananchi.
Amesema mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na vifaa ambavyo havihusiani na uchungaji kama vipande vya chupa, shanga, kwato za Ng’ombe, chupa tano za ubani na kifuu cha nazi vifaa hivyo vinatumika kutapeli watu wakati wa maombezi kuwaaminisha anatenda miujiza na vipande vya chupa vinatoka kinywani mwa binadamu.
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linatoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha mavuno na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kuwakamata watuhumiwa hao na kuwafikisha katika vyombo vya dola..
Imeandaliwa na
Jamila ismail
Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 13,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa