Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Arusha zimeibuka vinara katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2018/19.
Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati wa kutoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2018/19.
Waziri Jafo amebainisha kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa kukusanya mapato ghafi yaani Fedha nyingi kuliko Halmashauri zote nchini; Jiji hilo limefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh Bil 14.4 kati ya bajeti yao ya kukusanya Tsh Bil 68.6. Makusanya hayo ni sawa na aslimia 21 ya malengo waliyojiwekea.
Wakati huo huo Arusha inaongoza kwa kukusanyanya vizuri kiasilimia na imefanikiwa kukusanya mapatyo kwa asilimia 26 ya malengo waliyojiwekea; Hii ni kwamba Jiji la Arusha limekusanya kiasi cha Tsh Bil. 4.1 kati ya Tsh Bil.15.6 ya malengo yao ya makusanyo kwa mwaka wa Fedha 2018/19.
“Ieleweke wazi kuwa Jiji la Arusha ndio lililofanya vizuri kimakusanyo kwa mujibu wa asilimia lakini Jiji la Dodoma ndio lililokusanya Fedha nyingi zaidi kuliko halmashauri zote Tanzania alisema Mhe. Jafo.
Aliongeza kuwa kwa upande wa Halmashauri za Manispaa iliyofanya vizuri zaidi ni Manispaa ya Musoma na kwa Halmashauri za Mji zimeongozwa na Mbinga na upande wa Halmashauri za Wilaya zimeongozwa na Kisarawe.
Mhe Jafo alitanabaisha kuwa kwa makusanyo hayo ukiyawekwa Kimkoa inaongozwa na Mkoa wa Simiyu ikifuatiwa na Manyara, kisha Lindi, Mara, Pwani, Arusha, Njombe,Dodoma, Mwanza na kumalizia na Geita.
Mhe Jafo aliweka wazi pia Halmashauri zilizofanya vibaya zaidi kwa kukusanya chini ni Halmashauri ya Wilaya ya Masasi DC, Nanyamba TC, Nanyumbu DC, Newala Dc,Tandahimba Dc,Songea Dc,Madaba Dc, Rorya na Morogoro Dc.
Na kwa Upande wa Mikoa iliyofanya vibaya kwa kukusanya mapato kidogo ni Mkoa wa Mtwara, Ruvuma na Kigoma.
Waziri Jafo aliwakumbusha viongozi wanaohusika kuwa ukusanyaji wa mapato ndio kitakua kigezo cha kupimwa katika utendaji kazi wao hivyo kila mtu ajitathmini kulingana na mapato ya Halmashauri/Mkoa wake.
Kwa mwaka wa Fedha 2018/19 Halmashauri zilipangiwa kukusanya Tsh Bil. 735.6 kutoka kwenye vyanzo vyake vua ndani na hadi kufikia tar 30 Septemba.2018 Halmashauri zilikusanya jumla ya Tsh Bil 143.6 sawa na asilimia 20 ya makisio ya mwaka. Kwa mwaka wa fedha 2017/18 Halmashuri zilipangiwa kukusanya Tsh Bil. 687.3 na hadi kufikia septemba 30 mwaka 2017 ziliweza kukusanya Tsh. Bil 126.8 sawa asilimia 18 ya makisio ya mwaka.
“Kutokana na Takwimu hizo inaonyesha kwamba Halmashuri zimeongeza wingi wa mapato kwa kiasi cha Tsh Bil. 16.7 na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani umeongezeka kwa asilimia 2” alisema Jafo.
Imandaliwa na Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
|
|
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa