• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

JOTO kuongezeka duniani hadi nyuzi 1.5

Tarehe ya kuwekwa: October 10th, 2018

JOPO la kiserikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC, limetoa ripoti maalum leo ikionya kuhusu madhara ya kukosa kufikia lengo hilo, miezi miwili kabla ya mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi. Tathmini hiyo inaonesha kuwa waangalizi wameona athari za mabadiliko ya nyuzi 1, na kutaja mabadiliko hayo kuwa hali ya hewa iliyokithiri, kupanda kwa usawa wa bahari, na kupotea kwa barafu katika eneo la Arctic.

Chini ya ya lengo hilo, wataalamu wanasema usawa wa bahari hautapanda kwa zaidi ya sentimita kumi. Vile vile itapunguza uwezekano wa bahari ya eneo la Arctic lisilo na barafu msimu wa joto, na miamba ya matumbawe kupungua kwa kati ya asilimi 70 hadi 90, kinyume na kupotea kabisa iwapo joto litaongezeka kwa nyuzi 2.

Ripoti hiyo aidha inaonesha kuwa sera ya mabadiliko ni muhimu katika ardhi, kawi, viwanda, majengo, usafiri na miji, na kaboni dioksidi inayotolewa na binadamu inafaa kushuka kwa asilimia 45 kutoka viwango vya mwaka 2010 ifikapo mwaka 2030 ili kuafikia lengo la chini.

Mwenyekiti wa IPCC Hoesung Lee, amesema mabadiliko ya hali ya hewa yanawaathiri watu, mazingira na maisha yao kote duniani. ´´Kupunguza joto hadi nyuzi 1.5 inawezekana lakini itahitaji mapito yasiykuwa ya kawaida katika vipengele vyote vya jamii. Kuna manufaa ya wazi kwa kuweka kiwango cha joto hadi nyuzi 1.5 ikilinganishwa na nyuzi mbili au zaidi. Kila kiwango ha joto kina umuhimu.´´

Ripoti hiyo inasema viwango vya Kaboni Dioksidi vinafaakufikia kile alihokiita ´´net zero´´ ifikapo mwaka 2050 . Hii ina maana gesi itakayotolewa inafaa kuondolewa hewani, kwa kutumia technolojia inayojulikana kama kukamatwa kwa kaboni ambayobado ni changa.

Makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 yaliangazia juhudi za kuhakikisha kuongezeka kwa joto kunasalia chini ya nyuzi mbili na kuzingatia mbinu za kudhibiti ongezeko la joto hata zaidi hadi nyuzi 1.5. Marekani ambayo ni mtoaji mkuu wa Kaboni Dioksidi ilijitoa kwenye mkataba huo wa Paris mwaka uliopita, hivyo kuzua wasiwasi kuhusu ufanisi wake.

Watafiti wengi wanasema iwapo hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa kupunguza utoaji wa gesi, dunia itaendelea kupitia njia ya joto la dunia ambayo inaweza kufika nyuzi 3 au 4. Mawaziri wa mazingira wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukamilisha majadiliano  kuhusu misimamo yao katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa ya Desemba jijini Katowice, Poland, kuhusu utekelezaji wa mkataba wa mwaka 2015.

Kamishna wa Masuala ya Hali ya Hewa wa Umoja wa Ulaya Miguel Canete alitaka kuongeza lengo la mwaka 2030 hadi asilimi 45 ikilinganishwa na mwaka 1990, lakini hatua hiyo imepingwa na Ujerumani na mataifa mengine wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Mwandishi: Sophia Chinyezi/DPAE

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa