Ripoti mpya ya jopo la ushirikiano wa serikali za dunia juu ya mabadiliko ya hali ya hewa yaonya kwamba joto linaogezeka kwa kasi kubwa duniani kuliko ilivyotabiriwa.
Ikiwa kasi ya kuongezeka kwa joto hilo haitadhibitiwa na kupunguzwa kwa kiwango kikubwa jopo linaeleza kwamba hatari zinazo tokana na hali ya hewa kwa binadamu, mfumo wa mazingira na maendeleo endelevu zitaongezeka kwa kiwango kisichoweza kubadilishwa tena.
Hatua gani zichukuliwe?
Hatua zinazo paswa kuchukuliwa zilielezwa wakati wa mkutano wa Paris juu ya kupunguza hali ya joto duniani, katika mkataba ambao Marekani imejiondowa .
lakini mwandishi wa sauti ya amerika mjini Geneva Lisa Schlien anaripoti kwamba wanasayansi wa jopo la kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa wanatuarifu kuwa kuongezeka kwa joto duniani tangu mwanzo wa enzi ya viwanda imeongezeka kwa zaidi ya nyuzi moja centigrade pekee yake.
Lakini katika kiwango cha sasa cha uchafuzi wa hewa kwa gesi za sumu za carbon maarufu kama greenhouse gases wanasayansi wanasema kiwango cha joto kitafika nyuzi moja nukta 5 mnamo miongo kadhaa ijayo.
Ripoti yao inaeleza kwamba inabidi kwa nchi za dunia kuzuia kabisa hadi sufuri uzalishaji wa gesi za carbon ili kuzuia kuongezeka kwa joto.
Inaonya kwamba kuongezeka kwa nyuzi mbili zaidi kutaongezea kwa kiwango kikubwa majanga ya kiasili, kuharakisha kuyayuka kwa barafu katika bahari ya Arctic , na kusababisha visiwa kutoweka chini ya bahari inayopanda na kusababisha hali ambayo itakua vigumu kuzalisha chakula cha kutosha kulisha wakazi wanaoongezeka duniani.
Katibu mkuu wa shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa Petteri Taalas anasema bado kuna muda kwa watu kubadili tabia kuweka viwango vya gesi za carbon kuwa chini.
Anasema kupunguza joto la dunia kupanda kwa hata nusu nyuzi centigrade kutaleta mabadiliko makubwa
Njia ya kuepusha janga la dunia
Moja kati ya suala kuu ni kwamba kutakuwepo na watu milioni 420 ambao hawato taabika kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa tutaweza kudhibiti kiwango cha joto kubaki chini ya nyuzi moja nukta tano.na tuna maeneo kadhaa ya dunia ambayo yako hatarini sana.
Visiwa vidogo, kanda ya Mediterranean na nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara tayari yako mashakani na yatadhurika zaidi siku za mbele.
Taalas anapendekeza hatua kadha za kuchukuliwa na serikali na watu binafsi ili kupunguza kiwango cha joto duniani ikiwa ni pamoja na kusitisha matumizi ya mafuta ghafi yanayo patikana chini ya ardhi ambayo ndio yanayo sababisha uchafuzi mkubwa.
Anasema nishati ya jua , umeme kutokana na maji nishati kutokana na upepo na aina nyingine za nishati zinabidi kutumika na kukidhi mahitaji ya nishati ya watu. Anaeleza inabidi pia kuhimiza utumaiji wa magari na mabasi ya umma yanayotumia nishati ya umeme. Anasema serikali zina mwanya wa miaka 30 kusitisha utumiaji wa mafuta machafu na kupunguza joto kuongezeka kwa nyuzi 1.5
Imetayarishwa na Mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa