MRADI wa ujenzi wa zahanati ya Lupapila Kata ya Subira Manispaa ya Songea umegharimu kiasi cha Tsh.40,000,000.
Mtendaji kata Subira Alexander Kapinga ametoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Lupapilakwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Kapinga amesema kati ya fedha hizo Tsh.36,000,000 ni fedha kutoka Halmashauri na Tsh.4,000,000 ) ni nguvu za Wananchi ,ujenzi huu unatarajiwa kukamilika mwaka huu wa fedha ambapo Tsh.20,000,000/= (milioni ishirini) imetengwa.
Kapinga amesema kata ya Subira ni miongoni mwa Kata 21 zilizopo Manispaa ya Songea ambapo ina jumla ya mitaa 8 na wakazi 8876 kati yao wanaume wapo 4402 na wanawake 4474, shughuli za kiuchumi zinazofanyika ni Kilimo ,Ufugaji ,Uvuvi na Biashara ndogondogo.
Ameendelea kuzungumza kuwa ujenzi huu uliibuliwa na Wananchi wa mtaa wa Mahinya na Ngandula kata ya Subira baada ya kukosa huduma za kiafya ambapo Wananchi walianza kwa kufyatua tofali 28,000 na mmoja alijitolea eneo kwaajili ya ujenzi ambao ulianza 25/5/2010.
“Lengo la mradi huu ni kurahisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wakazi wa Lupapila wapatao 2452 na mitaa jirani kama vile Subira kati, Nangwahi na Muungano”.Amesema Kapinga.
Pia baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati hii tunatarajia kuanza ujenzi wa Zahanati nyingine katika mtaa wa Muungano ambao hupo mbali na upatikanaji wa huduma za afya.
Imeandaliwa na
Jamila myovela
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Septemba 2, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa