• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KADI ya Afya ya CHF iliyoboreshwa kutumika katika mkoa mzima

Tarehe ya kuwekwa: May 8th, 2018

MWANACHAMA aliyejisajiri katika Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) kupitia CHF iliyoboreshwa anaweza kupata huduma za afya katika vituo vyote ndani ya mkoa.

Serikali imeamua kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) kutoka kutoa huduma katika Kituo walichojiandikishia na sasa kupata huduma za afya katika vituo vya huduma za afya vilivyopo ndani ya mkoa.

Akizungumza katika mafunzo ya siku tatu kwa washiriki 83 wa mafunzo ya CHF iliyoboreshwa toka vituo 20 vya Halmashauri ya Manispaa ya Songea,Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Anton Mhina amesema CHF iliyoboreshwa itamwezesha mwanachama kupata huduma ya afya kwenye kituo chake,hospitali za wilaya na mkoa.

Hata hivyo amesema ili kuhakikisha huduma zinapatikana kwa uhakika katika vituo vyote,mwanachama wa CHF hivi sasa atalipia kwa mwaka shilingi 30,000 badala ya 10,000 na kwamba serikali itachangia shilingi 30,000 hivyo kufanya kwa mwaka mzima CHF iliyoboreshwa kila kaya  kuchangiwa jumla ya shilingi 60,000.

“Katika CHF iliyoboreshwa kila kaya itasajiri watu sita wakiwemo wategemezi watano na Mkuu wa Kaya,kila mtegemezi atapewa kadi yake ya afya badala ya kadi moja kutumiwa na wote,baada ya kujisajiri haizidi siku mbili Mwanachama anakuwa amepata kadi yake’’,anasisitiza Mhina.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea Dk.Mameritha Basike amewataja washiriki wa mafunzo hayo toka Manispaa ya Songea kuwa ni wenyeviti wa kamati za afya za mitaa,wauguzi wa vituo vya afya,wahasibu na wawezeshaji wanane kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na TAMISEMI.

Ameyataja mafunzo ambayo yametolewa kwa washiriki hao kuwa ni CHF iliyoboreshwa,mafunzo ya utoaji wa fedha kwenye vituo na manunuzi ya dawa kupitia ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma.

Akizungumza wakati anafungua rasmi mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo ametoa rai kwa washiriki kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ili kutoa habari sahihi kwa wananchi kuhusu manufaa ya CHF iliyoboreshwa.

CHF iliyoboreshwa ni Bima ya Afya kwa ajili ya wananchi wa  ambao hawana uwezo au hawajatimiza vigezo vya kujiunga na Bima ya Afya ya Taifa (NHIF).

CHF iliyoboreshwa imeanzishwa kuondoa changamoto zilizokuwepo kwenye mfuko wa afya ya jamii (CHF) ulioanzishwa mwaka 2001.

Imeandaliwa na Albano Midelo

Afisa Habari Manispaa ya Songea

Mei 8,2018

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa