Na;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI
MANISPAA YA SONGEA.
Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano ameiongoza kamati ya fedha na uongozi katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika sekta ya Afya na Elimu msingi na Sekondari iliyofanyika leo tarehe 12 agosti 2022.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa mabweni mawili na madarasa matatu yaliyopo kata ya Seedfarm katika shule ya Wavulana Songea (miradi SEQUIP) kwa gharama ya shilingi 260,000,000, mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kata ya Mletele (mradi wa Global fund) kwa gharama ya shilling 545,334,640, ujenzi wa mabweni mawili na madarasa matatu katiaka shule ya sekondari ya wasichana songea iliyopo katiaka kata ya Mjini (miradi SEQUIP) kwa gharama ya shilingi 280,000,000, pamoja na Mradi wa wa ujenzi wa kituo cha afya Tanga kilichopo katika kata ya Tanga (mradi wa serikali kuu) kwa gharama ya shilingi 500,000,000.
Akiongea kwa niaba ya Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mheshimiwa Jeremia Mlembe ambaye pia ni Naibu Meya Manispaa ya Songea, amewataka wataalamu wote kuendelea kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ikiwemo na kuhakikisha wanafuata kanuni ya manunuzi ya vifaa vya Serikali vya ujenzi.
MWISHO.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa