Mstahiki Meya Manispaa ya Songea mhe. Michael Mbano amewataka wataalamu wahakikishe wanasimamia utekelezaji wa miradi na kuikamilisha kwa wakati.
Hayo yamejiri wakati wa ziara ya kamati ya fedha na uongozi iliyoongozwa na Mstahiki Meya wa Manjispaa hiyo ambapo wamefanikiwa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ambayo inaendelea kujengwa ambapo wametembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Lami nzito yenye urefu wa KM 10.01 yenye thamani ya Bil. 10,01, ujenzi wa madarasa vyumba 5 na matundu ya vyoo 8 shule ya sekondari ya matogoro kwa thamani ya ujenzi wa shilingi Mil. 134,4.
Miradi mingine iliyotembelewa nipamoja na ujenzi wa madarasa 3 na matundu 8 ya vyoo shule ya sekondari ya Matarawe kwa thamani ya mil. 86.4, Ujenzi wa Zahanati ya matarawe pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Ruhuwiko, ujenzi wa shule ya Amali inayojengwa kwa bil. 1,6, pamoja na mradi wa ujenzi wa madarasa 11 na matundu ya vyoo 8 shule ya sekondari ya Ruvuma.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 22 januari 2025 kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa hatua za miradi maendeleo.
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa