Kamati ya fedha na Uongozi ikiongozwa na Naibu Meya Manispaa ya Songea Jeremiah Mlembe wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi 6 ya maendeleo ambayo inaendelea kujengwa katika kata Ndilima Litembo, Mletele, Tanga, Mjini, Lizaboni na Lilambo iliyofanyika tarehe 09 Mei 2024.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 2 na matundu 4 ya vyoo shule ya msingi Ndilima litembo inayojengwa kwa kiasi cha fedha Mil. 54,800,000 fedha kutoka EP4R, Ujenzi wa madarasa 7 sekondari ya Mdandamo fedha kutoka Serikali kuu kwa kiasi cha shilingi Mil. 170,500,000 na Ukamilishaji wa Hosptali ya Manispaa ya Songea inayojengwa kwa kiasi cha Mil. 800,000,000.
Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi inayojengwa kwa gharama ya Mil. 180,000,000, ujenzi wa madarasa10 na matundu 10 ya vyoo shule ya Sekondari Londoni kwa kiasi cha Mil. 259,500,000, Ujenzi wa vyumba vya madarasa 8 shule ya Sekondari Sili kwa kiasi cha 192,000,000 fedha kutoka Serikali kuu.
Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kukagua miradi na kutathimini utendaji wa kazi wa miradi hiyo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazoweza kukwamisha utendaji wa kazi wa miradi hiyo.
Aidha, pamoja na pongezi zilizotolewa na kamati kupitia hatua nzuri ya ujenzi wa miradi hiyo umetolewa wito kwa wataalamu wahakikishe wanasimamia kwa umakini miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati.
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa