Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali. Lengo la ziara hii ni kufanya ufuatiliaji wa hatua za miradi inayoendelea kutekelezwa.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na Ofisi ya Kata Ndilimalitembo ambapo Ujenzi umegharimu shilingi 10,235,318.23, fedha za mapato ya ndani, Shule ya Sekondari Matogoro Ujenzi wa madarasa 5 na matundu 8 ya vyoo, ukigharimu shilingi 134,400,000 kutoka Serikali kuu, Shule ya Sekondari Mashujaa Ujenzi wa darasa 1 na matundu 8 ya vyoo, fedha kutoka Serikali kuu, Shule ya Sekondari Bombambili Ujenzi wa madarasa 4 na matundu 8 ya vyoo, ukigharimu shilingi 110,400,000 kutoka Serikali kuu, Kata ya Llilambo Ujenzi wa jengo la viwanda (Machinga) kwa shilingi 15,000,000, fedha za mapato ya ndani.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Mheshimiwa Michael Mbano, akizungumza katika ziara hiyo, amewataka wataalamu kuendelea kutenga bajeti ili kukamilisha majengo mbalimbali ambayo tayari yamejengwa lakini bado hayajakamilika.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuongeza jitihada katika kusimamia miradi ili iweze kukamilika kwa wakati.
Ziara hiyo ilifanyika leo tarehe 22 Oktoba 2024 na ilihudhuriwa na wajumbe wa kamati pamoja na Menejimenti ya watumishi, Kamati inaendelea kuhamasisha ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Songea.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa