Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa ya Songea, Imefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata za Msamala, Mjimwema na Mshangano.
Ziara hiyo imelenga kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika kata hizo pamoja na kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa kulingana na malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mstahiki Meya Mhe. Abraham Mbunda amewataka wataalamu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kusimamia kwa karibu miradi yote ya maendeleo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa, ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi.
Ziara hiyo imehusisha Waheshimiwa Madiwani wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Manispaa ya Songea. Ziara hiyo imefanyika tarehe 20 Januari, 2026.
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa