• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMATI ya Fedha na Uongozi yaridhishwa na kasi ya ujenzi wa stendi mpya Songea

Tarehe ya kuwekwa: June 27th, 2018

KAMATI ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kukagua stendi mpya mabasi katika eneo la Kata ya Tanga nje kidogo ya Manispaa ya Songea.Mara baada ya ukaguzi kamati imeridhishwa na hatua ya ujenzi unaofanywa na Kampuni ya China Sichuan International.mradi umeanza Mchi 25,2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2018.Mradi katika awamu ya kwanza unagharimu zaidi ya bilioni sita ambapo tayari mradi umefikia asilimia 14.

Kazi ambazo zinafanyika awamu ya kwanza katika stendi hiyo ni ujenzi wa lami nzito yenye kilometa mbili,taa barabarani,maduka 30,vibanda 20 vya tiketi,jengo la utawala,vyoo vya matundu 12 na eneo la kupaki magari.Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo hadi sasa Mkandarasi amelipwa zaidi ya shilingi bilioni 444.

mradi hadi kukamilika unatarajia kugharimu shilingi bilioni 12  ambapo katika awamu ya kwanza, zitatumika shilingi bilioni sita na kwamba  stendi mpya ya mabasi inatarajia kuanza kazi baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya utekelezaji ambayo ni kuanzia Oktoba 2019.

Ili kuendana na kasi ya ukuaji wa mji,Manispaa iliamua kutenga eneo la kujenga kituo kikuu cha mabasi kuwa Kata ya Tanga ikiwa ni umbali wa takribani kilometa 14 toka mjini Songea.Kazi nyingine ambazo zitafanyika katika awamu ya kwanza na pili ya mradi huo kuwa ni kujenga barabara za kuingia na kutoka stendi zenye kiwango cha lami nzito,kujenga mirefeji ambayo  itapeleka maji mtoni,ujenzi wa eneo la stendi lenye ukubwa wa meta za mraba 32,914,kuweka taa za barabarani katika eneo lote la stendi,eneo la utawala na kujenga majengo yenye hoteli za kisasa.

Fedha za mradi wa stendi zimetolewa kupitia Benki ya Dunia,jumla ya hekari 15 zimetwaliwa katika eneo hilo ili kupitisha stendi,ambapo shilingi milioni 38 tayari zimelipwa kama fidia kwa wananchi.

Imetolewa na Albano Midelo

Afisa Habari Manispaa ya Songea

Juni 27,2018

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa