KAMATI ya Fedha na Uongozi Manispaa ya Songea ikiongozwa na Mstahiki Meya Michael Mbano amewataka wataalamu kuhakikisha wanasimamia miradi kikamilifu na kukamilika kabla tarehe 30 juni 2023.
Agizo hilo limetolewa katika ziara ya kamati ya Fedha na Uongozi inayoendelea kufanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 11 hadi tarehe 12 Mei 2023 kwa lengo la kukagua miradi miradi ya maendeleo ili kulinganisha hali ya mradi na thamani ya fedha.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa leo ni pamoja na mradi wa ukamilishaji wa chumba 1 cha darasa shule ya Msingi Ruvuma kwa thamani ya Mil. 18,750,000 fedha kutoka Serikali kuu, ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 2 Shule ya Msingi Mbulani kwa thamani ya Mil. 25,000,000 kutoka Serikali kuu, Ukamilishaji wa Madarasa 2 Shule ya Msingi Kipera kwa thamani ya Mil. 20,000,000 fedha za mapato ya ndani, na Ujenzi wa Uzio wa Bweni la watoto wenye mahitaji maalumu Shule ya Msingi Subira kwa thamani ya Mil. 60, 000,000 fedha ktoka Serikali kuu.
Miradi mingine ambayo imetembelewa ni pamoja na ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa LAMI kwa thamani ya Mil. 15,000,000 fedha kutoka mapato ya ndani, ukamilishaji wa matundu 10 ya vyoo Shule ya Msingi Muungano kwa thamani ya Mil. 5,000,000 fedha kutoka mapato ya ndani, Ukamilishaji wa madarasa mawili 2 Shule ya Msingi Londoni kwa thamani ya Mil. 25,000,000 kutoka Serikali kuu, Ujenzi wa madarasa 2 Shule ya Msingi London kwa thamani ya Mil. 20,000,000 fedha kutoka mapato ya ndani, na ukamilishaji wa bweni 1 la Shule ya Sekondari ya Wavulana kwa thamani ya Mil. 22,000,000 fedha kutoka Serikali kuu.

Aidha Miradi mingine ni ukamilishaji wa matundu 10 ya vyoo shule ya Msingi Likuyufusi kwa thamani ya Mil. 10,000,000 fedha kutoka Serikali kuu, ukamilishaji wa madarasa mawili Shule ya Msingi Sabasaba kwa thamani ya Mil. 25,000,000 fedha kutoka Serikali kuu, Ukamilishaji wa Maabara Shule ya Sekondari Matarawe kwa thamani ya Mil. 12,000,000 fedha za mapato ya ndani, pamoja na ukarabati wa Ofisi ya Kata ya Matarawe kwa thamani ya Mil 5,000,000 fedha za mapato ya ndani.
Mhe Mbano ametoa pongezi kwa wataalamu hao kupitia utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo huku akiwataka kuzingatia miradi iendane na thamani ya fedha.
Ziara hiyo itahitimishwa kesho tarehe 12 Mei 2023 kwa kutembelea kata ya Tanga, Mshangano, na kata ya Mletele.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa