Kamati ya fedha na uongozi ikiongozwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano amewataka wataalamu kuhakikisha wanakamilisha miradi mbalimbali ya ujenzi ambayo bado haijakamilika ili iweze kutumika kama ilivyokusudiwa.
Kamati hiyo imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Lukala uliotekelezwa kwa shilingi Milion. 48 fedha za EP4R, Ukamilishaji wa maboma 3 katika shule ya Sekondari ya Lukala uliotekelezwa kwa Mil.37,500.000 fedha za SEQUIP pamoja umaliziaji wa matundu 10 ya vyoo Lukala Sekondari wenye thamani ya milion. 10.
Miradi mingine iliyotembelewa na kukaguliwa ni ukamilishaji wa madarasa 2 shule ya msingi Mkuzo shikizi inayojengwa kwa milion 16 fedha za mapato ya ndani, Ujenzi wa madarasa 8 shule ya Sekondari Sili yenye thamani ya Mil.192,000,000 fedha kutoka Serikali kuu, kutembelea eneo la ujenzi wa maegesho ya malori ambao unatarajia kujengwa wenye thamani ya Mil. 250, pamoja na ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi inayojengwa kwa thamani ya Mil. 180,000,000 fedha kutoka Serikali kuu.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 25 Julai 2024 ambayo imeshirikisha wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi, na wataalamu.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa