Kamati ya Siasa Wilaya ya Songea Mjini imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa lengo la kukagua hatua mbalimbali za ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 06 Mei 2025 ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Songea Mjini Mwinyi Msolomi ambapo walitweza kutembelea mradi wa maengesho ya Malori kata ya Lilambo A, Ujenzi wa duka la dawa katika kituo cha afya Mjiwemema, Ujenzi wa Sekondari ya Ruhuwiko pamoja na Mradi wa Maji kata ya Matogoro ambapo miradi hiyo inatarajia kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2025.
Msolomi amewapongeza wataalamu wa Manispaa ya Songea kwa kusimamia miradi kwa ubora zaidi ambapo pia miongoni mwa miradi hiyo ipo katika hatua mbaloimbali za ukamilimshaji. “alipongeza”
Na,
AMINAPILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa