KAMATI ya Siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Ruvuma, wakiongozwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bi Christina Mdeme wamekagua mradi wa standi kuu ya Mkoa inayojengwa kata ya Tanga Manispaa ya Songea.
Akitoa taarifa kwa wajumbe wa kamati ya siasa Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea,Nicholaus Danda amesema mradi unatarajiwa kukamilika mwezi septemba,2019 ambao umegarimu Zaidi ya Bilioni 6,189 na mpaka sasa mkandarasi ameshalipwa Zaidi ya Bilioni 3,606 na mradi umefika asilimia 80 ya utekelezaji.
Danda ameyataja malengo ya kujenga standi hiyo ni kupunguza msongamano wa magari,kuboresha sekta ya usafirishaji,kupanua mji na kuongeza Ajira, kujenga barabara katika kiwango cha lami nzito km 2 umefikia asilimia 70.
Ameyataja malengo mengine kuwa ni ujenzi wa mfereji asilimia 40, sehemu ya kuegesha magari asalimia 90,vyumba vya maduka 30 vimefikia asilimia 95,vyumba vya kukatia tiketi 20 vimefikia asilimia 95,jengo la utawalalimefika asilimia95, ujenzi wa choo cha umma umefikia asilimia 90,ujenzi wa sehemu za kukaa abiria umefikia asilimia 95,kuvuta umeme wa Tanesco asilimia100, Taa za barabarani (SOLAR)asilimia 10.
”Mhandisi Mshauri wa mradi huu ni kampuni ya BICO-Bureau for Industrial Cooperation kwa gharama Zaidi ya Bilioni 319,Mkataba na LGA/103/2017/2018/C/102 ambao umeanza tarehe 25 Machi,na unatarajiwa kumaliza muda wake septemba 30,2019.Mpaka sasa Mkandarasi amelipwa Zaidi ya Bilioni 229,”.amesema Danda.
Naye,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mdeme ameshauri katika eneo la standi waweke sehemu ya kupaki Pikipiki,Bajajina kila eneo kuweka mabango yatakayoweza kumjulisha mtu akae katika eneo lake.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Chama cha Mpinduzi (CCM) Odo Mwisho ameshauri wabadilishe mita za umeme ambazo zimewekwa kwenye fremu za maduka zisiwe za kuchangia kila chumba kiwe na mita yake ili kuepusha migogoro hapo badae,ni vizuri kuwasiliana na Halmashauri ya Mnispaa ili kutatua bajeti ndogo waliyokuwanayo.
Tanzania imepokea mkopo toka Benki ya Dunia Chini ya kuzijenga serikali za mitaa (Urban Local Government Strengthening Program (ULGSP) mpango huu ili kuendeleza miundombinu ya miji 18 ya Tanzania Bara. Miji ambayo inafaidika na mpango huu ni Songea, Sumbawanga, Singida, Tabora ,Shinyanga, Musoma, Moshi, Bukoba ,Lindi, Morogoro, Iringa, Babati, Masasi , Kibaha, Njombe , Mpanda, Korogwe na Geita.
Imeandaliwa na
Farida Mussa
wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea.
Agosti 29,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa