Kamati ya siasa wilaya ya Songea kupitia mwenyekiti wa ccm wilaya Mh. Mwinyi Msolomi imempongeza mkurugenzi wa manispaa ya songea bashiru muhoja nawatendaji wake kwa kuweza kumaliza baadhi ya miradi katika Manispaa hiyo na mingine kufikia hatua za mwisho za kumalizika.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya serikali katika manispaa ya songea akiambatana na kamati ya siasa wiliya ambapo Mh. Msolomi Amempongeza mkurugenzi wa manispaa ya songea na watendaji wake kwakumaliza baadhi ya miradi kiustandadi na mingine kufukia hatua za mwisho, pia amempongeza mkurugenzi kwa kuweza kuipeleka miradi hiyo nje ya mji kwasababu itasaidia kupanuka kwa mji kwa wananchi kufuata maeneo hayo kwa sababu ya miundombinu bora itakayo wavutia.
Aidha kupitia ziara hiyo Mh. Msolomi amemtaka mkurugenzi na watendaji wake kuepuka kumtumia mkandarasi mmoja katika kusimamia miradi yote bali kugawa miradi hiyo kwa wakandarasi tofauti tofauti hii itasaidia kurahisha miradi hiyo kumalizika kwa wakati, kwasababu mkandsarasi anapopata changamoto kwenyue mradi mmoja mingine itakua inaendelea lakini ukimtumia mkandarasi mmoja akipata changamoto basi miradi yote anayo isimamia itakwama na haitamalizika kwa wakati.
Hata hivyo mh. Msolomi amewataka wakandarasi wanao simamia miradi hiyo kuwajali wafanyakazi wa kitanzania kwakuwalipa kufuatia sheria za nchi zinavyotaka na kupewa haki zao zote ili weaweze kujikwamua kiuchumi na sio kuwakandamiza, hii itasaidia pia kwa miradi hiyo kuacha faida kwa vijana wakitanzania wanaofanya kazi katika miradi hiyo.
Mh. Mwinnyi Msolomi amemshukuru mkurugenzi kwakuweza kuisimamia miradi hiyo kwa uaminifu na weledi mkubwa nakumalizika kwa mpaka kwaubora unaostahili , kwahiyo yeye na kamati ya siasa wameridhishwa na miradi hiyo iliyomalizika na wamemwomba hiyo iliyobaki iweze kukamilika kwa ubora uleule.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa