KAMATI ya Ushauri ya TEHAMA katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,imefanya kikao maalum cha ikijadili masuala mbalimbali yanayohusu TEHAMA.Kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye ukumbi mdogo wa Manispaa ya Songea kimeongozwa na Mwenyekiti wake Christopher Ngonyani na Katibu wake Azizi Makaburi .Agenda muhimu zilizojadiliwa katika kikao hicho zilikuwa ni kueleza majukumu ya kamati,kupitia mifumo ya malipo,kufanya tathmini ya vifaa vya kukusanyia mapato(POS) na kujadili mifumo,miundombinu ya TEHAMA iliyopo katika Manispaa ya Songea.
Pia kamati hiyo imedhamiria kuona sera za TEHAMA zinakwenda sanjari na mpango mkakati,kutengeneza na kupitia sera ya matumizi bora na sahihi ya TEHAMA na kuhakikisha kuwa sera ya TEHAMA ya Halmashauri ya Manispaa inaboreshwa kwa kufanyiwa mapitio,kuratibu matumizi ya mifumo na kufanya ziara ya vitendo kwa kutembelea mifumo ya TEHAMA zaidi ya tisa iliyopo katika Manispaa ya Songea hali ambayo itawajengea uwezo kamati hiyo kuhusu mifumo hiyo na changamoto zake ili kutoa ushauri wa kukabilina na changamoto husika.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa