Kampuni ya kimataifa ya serikali ya China inayoitwa SIETICO inaendelea na kazi ya ukarabati wa barabara za Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma kwa kiwango cha lami nzito. Kampuni hiyo imeingia mkataba wa miezi 18 kukarabati barabara zenye urefu wa kilometa 10.3 zilizogharimu zaidi ya sh.bilioni 10.96.Mkataba huo unaanzia Machi 25,2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2019.Uchunguzi ambao umefanywa katika moja ya Barabara àmbazo zinakarabatiwa ya FFU hadi Matogoro umebaini kuwa Kampuni ya SIETICO inaendelea na kazi ambayo wamesema wanatarajia kukamilisha kabla ya mwisho wa mkataba. Kukamilika kwa barabara hizo kwa kiwango cha lami itakuwa ni moja ya kichocheo cha maendeleo kwa watu wa manispaa ya Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa