Kata ya Matogoro nimiongoni mwa kata 21 zilizopo ndani ya Manispaa ya Songea ambayo imekuwa ikitekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kushirikisha wananchi na Wadau katika kutatua changamoto za miundombinu ya Elimu, Afya kwa lengo kuunga Mkono Jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika kutatua changamoto hizo kwa kushirikiana na wataalamu, wananchi na uongozi wa kata wameweza kutengeneza Madawati 382 kwa kupitia nguvu za wananchi, na madawati 120 mchango kutoka kwa Mhe. Diwani sawa na jumla ya madawati 502 kwa ajili ya shule Sekondari na Shule ya Msingi Matogoro.
Hayo yamejili wakati wa kukabidhi madawati kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea iliyofanyika kwenye mkutano wa hadhara ambao ulihudhuriwa na wananchi, viongozi wa vyama vya Siasa, Wataalamu na Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Matogoro tarehe 17 Mei 2023.
Akipokea madawati hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko alisema “ Niwa jibu wa Serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata miundombinu bora ya kusomea na kijifunzia ikiwemo na madawati, viti, meza na madarasa ambapo katika kutekeleza wajibu huo Serikali ilitoa fedha Bil 1.52 kujenga madarasa 76 na madawati 3800 ili kuboresha mazingira ya Elimu.
Akitoa pongezi kwa Uongozi wa Kata ya Matogoro kwa uzalendo uliotukuka kwa kutengeneza madawati/Viti na Meza 502 kwa lengo la kuondoa upungufu wa madawati kwa wanafunzi, utoaji wa chakula shuleni nauanzishaji wa Benk ya madawati. “Aliwapongeza.”
Dkt. Sagamiko aliongeza kuwa, Diwani wa kata ya Matogoro ni kiongozi mwenye mfano wa kuigwa kwa kuwa hupenda kushirikisha jamii yake anayoitawala katika kutanzua changamoto za kata yake bila kusubili mchango kutoka Halmashauri, hivyo amewataka Watendaji wa kata nyingine kuja kujifunza namna wanavyo fanikiwa katika utendaji wa kazi hususani usimamiaji bora wa miradi na kukamilisha ujenzi wa miradi kwa wakati. “Alibainisha na kusisitiza.”
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Matogoro Issa Mkwawa alisema “ Kutokana na upungufu uliojitokeza wakati anaingia madarakani kwa kupitia Wataalamu wake waliandaa Mpango Mkakati kuanza kuweka Benk ya Madawati kwa ajili ya Shule za Msingi na Shule za Sekondari ili kuondoa tatizo la madawati ambao hadi kufikia tarehe 17 Mei 2023 wameweza kutengeneza madawati 502 ambayo yamekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea. “Aliwashukuru”.
Naye Afisa Elimu kata ya Matogoro Samson Mbunda alisema Shule ya Sekondari Matogoro ina jumla ya wanafunzi 1080, na shule ya Msingi Matogoro ina jumla ya Wanafunzi 1252 ambapo kutokana na ushirikiano kutoka kwa wananchi, pamoja na Diwani wa Kata hiyo wameweza kutengeneza viti 502 ambayo yamekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea kwa ajili ya matumizi ya shule husika hivyo kwasasa hakuna upungufu wowote wamadawati.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa