Katibu wa Chama Cha Mapinduzi “CCM” Wilaya ya Songea Mjini James Mgego amewataka watumishi kufanya kazi kwa weledi ikiwemo na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ili kuwajengea Imani wananchi katika Serikali yao.
Mgego alisema Watumishi hufanya kazi kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutekeleza majukumu ambayo yapo katika kikanuni na miongozo mbalimbali ya kiutumishi wa umma.
Hayo yamejili katika kikao kazi cha watendaji wa Mitaa na Kata pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo kilichofanyika tarehe 09 novemba 2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kujitambulisha kwa watumishi hao.
Amewataka wataalamu kuendelea kutoa ushirikiano kwa wanasiasa ili kuleta maendeleo yenye tija kwa wananchi na kuondoa mgogoro ambao unaweza kukwamisha shughuli za maendeleo kwa jamii.
Ametoa rai kwa wataalamu wa Idara ya maendeleo ya jamii kuhakikisha wanasimamia majukumu yao ipasavyo kwa kuzingatia kanuni, na taratibu zilizowekwa katika kusajili vikundi na kuhakikisha wanakusanya fedha za madeni ya vikundi ambavyo havirejeshi mkopo kwa wakati kwa visigizio vya mikopo ya vikundi vya chama cha Mapinduzi. ‘Alisema Mgego’
Aliongeza kuwa mikopo ya vikundi iliyotolewa ni kwa ajili ya wanawake 4% vijana 4% na walemavu 2% ambayo ipo kwa mujibu wa kisheria na huzingatiwa maandiko na makubaliano ya mkataba wa mikopo lakini haina mahusiano na chama na alisema endapo vikundi hivyo vipo ameagiza vifuatiliwe na virejeshe mikopo hiyo mara moja ili waweze kukopeshwa wanavikundi wengine wenye sifa. Alisisitza.
Naye Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema alisema Wilaya ya Songea imegawanyika katika sehemu kuu mbili za kichama ambayo ina Wilaya ya Songea Mjini na Songea Vijijini ikiwa kwa upande wa Serikali imeagawanyika katika sehemu tatu 3 ambayo ni Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na Halmashauri ya Manispaa ya Songea zenye majimbo matatu 3 ya uchaguzi ikiwa na jumla ya Waheshimiwa Wabunge 6 kati yao watatu 3 ni kuchaguliwa na watatu 3 ni viti maalmu.
Pololet amewataka wataalamu wa Maendeleo ya jamii kuendelea kusimamia vikundi vyote vyenye madeni kwa kuzingatia makubaliano yaliyoandikwa kwenye mradi husika ili kuwezesha kuendelea kukopesha wanavikundi wengine.
Ametoa Rai kwa watendaji kata na mitaa kusimamia ujenzi wa madarasa 76 ambao unaendelea kutekelezwa Wilayani humo na kutoa agizo la kuhakikisha vyumba vya madarasa vinakamilishwa na kukabidhiwa ifikapo tarehe 30 Novemba 2022.
AMINA PILLY.
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa