Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba amefanya uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa dawa za kinga tiba ya Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo na Usubi, Matende, Minyoo na Mabusha katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Zoezi hilo hufanyika kila mwaka Kitaifa chini ya Wizara ya Afya kwa kushirikiana na RTI, ambapo kwa Manispaa ya Songea zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 16 Agosti 2023 hadi 202 Agosti 2023 katika kata zote 21 na Mitaa 95 kwa walengwa wenye umri kuanzia miaka 5 na kuendelea isipokuwa kwa Akina mama wajawazito, wagonjwa na watoto chini ya miaka mitano.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mnamo tarehe 16 Agost 2023 ambapo amewataka wananchi kushiriki katika zoezi la unywaji wa dawa kinga tiba za magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwani hazina madhara yoyote.
Alisema zoezi hilo linasimamiwa na wataalamu wa afya pamoja na wahudumu 1400 waliopewa mafunzo maalumu ya ugawaji wa dawa kutoka kila mtaa ambao watapita kwenye kaya 76,927 zilizopo ndani ya Manispaa ya Songea.
Kwa upande wake Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Bload Komba alisema “ kabla ya kuanza zoezi hilo watoa mafunzo kwa wataalamu pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi kupitia wenyeviti wa mitaa 95.
Alisema lengo la zoezi hilo ni unyweshaji wa kinga tiba kwa jamii kuwafikia wananchi kwa asilimia 80% kwa wananchi wasiopungua 286,285 kwa kaya 76,927 ambazo zitasaidia kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine, inauwa vimelea, kuepusha upungufu wa damu mwilini, kuwa makuzi bora ya watoto, na kuboresha nguvu kazi kwa jamii.
Bload alibainisha Madhara ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ni pamoja na ulemavu wa ngozi, vifo, maumivu ya muda mrefu,huchangia umaskini na kudumaza uchumi wa kifamilia.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa