Hiki ndiyo kiwanda kikubwa kuliko chochote Kusini mwa Jangwa la Sahara.Kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Kusini mwa Tanzania kina uwezo wa kuzalisha tani za saruji milioni tatu kwa mwaka.Kiwanda hiki ambacho kinamilikiwa na bilionea wa Afrika Alhaji Aliko Dangote raia wa nchini Nigeria,kimetengeneza ajira rasmi na zisizokuwa rasmi kwa wakazi wa Mkoa wa Mtwara na watanzania kwa ujumla.Tangu kugundulika kwa Gesi asilia katika Mkoa wa Mtwara kumesababisha Mkoa kuanza kukimbia kiuchumi ambapo hivi sasa ujenzi wa viwanda unaendelea na wawekezaji wamewekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo za utalii,fedha na hoteli zenye hadhi ya kimataifa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa