KIJIJI cha Chunya kilichopo katika Kata ya Mpapa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kimefutwa rasmi kwa kuwa kipo ndani ya Hifadhi ya asili ya Ruhekei.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye akizungumza na wananchi wa kijiji hicho amesema muda wa miezi 15 ambao walipewa wananchi hao kubomoa nyumba zao na kuondoka kwa hiari umemalizika.Nshenye amesisitiza kuwa itakapofika Novemba 30 mwaka huu serikali ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya itaanza kazi ya kuwaondoa wananchi wote ambao watakuwa bado hawajaondoka.
Hifadhi ya misitu ya asili ya Ruhekei yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 2000 ilianzishwa kwa kutangazwa katika gazeti la serikali ya kikoloni mwaka 1938 ambapo kijiji hicho kilianzishwa ndani ya hifadhi hiyo bila kupata usajiri mwaka 1984.Diwani wa Kata ya Mpapa Adolf Mandele amemwambia Mkuu wa wilaya kuwa wananchi wamekubali kuondoka ndani ya hifadhi hiyo kwa hiari isipokuwa wameiomba serikali kuwapatia usafiri wa kubebea mizigo yao.
Kijiji cha Chunya kina kaya zaidi ya 50 zenye wakazi zaidi zaidi ya 100,kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji vitano ambavyo vinaunda kata ya Mpapa.Vijiji vingine ni Mitawa,Burma,Mitange na Mpapa.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari na Mwandishi wa serikali
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa