Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano ( pichani upande wa kushoto) ameongoza kikao kazi cha baraza la Madiwani kilichofanyika leo tarehe 21 Agosti 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea nakuhudhuriwa na wakuu wa Idara na vitengo, Watendaji wa kata, kwa lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa kila robo ya mwaka kutoka kwenye Kata na kuzijadili ili kutatua changamoto zinazozikabili kata ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Mkutano wa Baraza la Madiwani utakaofanyika tarehe 23 Agosti 2023.
Akijitambusha Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba ambapo amewataka waheshimiwa madiwani kuendelea kutoa ushirikiano kwa wataalamu katika ili kuleta Msukumo wa maendeleo katika jamii.
Aidha kupitia kikao hicho zimejadiliwa hoja mbalimbali kutoka kwenye kata na kutolewa ufafanuzi papo kwa papo kutoka kwa wataalamu.
Imeandaliwa;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa