“ simamieni asilimia 10% iliyobakia ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao hawajaripoti shule kwa kushirikisha Vikao vya kamati ya Maendeleo ya kata (WDC), Bodi za shule, Serikali za mitaa kwa kuhakikisha kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza anaripoti shule.”
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano katika Baraza la pili la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2022/2023 lililofanyika leo tarehe 16 Februari katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea ambalo limehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Wataalamu, viongozi wa vyama vya siasa na Wananchi mbalimbali kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa kutoka kwenye kamati za kudumu, na kuboresha utendaji kazi wa Halmashauri.
Mheshimiwa Mbano amewataka wataalamu na Madiwani kuwajibika kila mmoja katika eneo lake ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Serikali sambamba na kusimamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa. “Alisisitiza”
Ametoa wito kwa viongozi na wataalamu, kusimamia miradi ipasavyo na endapo kutatokea chanagamoto yoyote inayokwamisha utendaji wa kazi wa mradi unashauriwa kupeleka taarifa kwa mkuu wa Idara husika ili kutatua changamoto hiyo sambamba na miradi yote iliyokamilika itumike na wasiwe waanzishaji wa miradi bila kukamilisha mradi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Alto Liwolelu amesema Halmashauri ya Manispaa ya Songea imeanza kutekeleza mkakati waliojiwekea wa kupeleka fedha Mil. 20 kila kata kwa kata 21 zenye jumla ya shilingi Mil. 420 fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kutatua changamoto zilizojitokeza katika kata husika.
Alto aliongeza kuwa fedha hizo hupelekwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi husika pia hutekelezwa kwa kuzingatia miradi vipaumbele walivyojiwekea na hukaguliwa kwa ajili ya kujiridhisha tahamani ya fedha . “Alibainisha”
Aidha, Kwa upande wa Waheshimiwa Madiwani walianza kwa kuwapongeza wataalamu kwa kwa kupanga bajeti ya Mil. 20 za kupeleka kwenye kila kata ambazo zinakwenda kutatua chanagamoto za eneo husika.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa