Na,
Amina Pilly.
Mstahiki Meya manispaa ya songea, Mhe. Michael Mbano ametoa wito kwa wawekezaji wote kuja kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji hususani katika sekta ya kilimo cha mahindi ya njano mkoani Ruvuma.
Wito huo umetolewa jana tarehe 29 agosti 2022 katika mkutano wa ufunguzi wa fursa za uwekezaji uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa dhumuni la kustawisha uwekezaji katika sekta ya kilimo mkoani Ruvuma ambao ulihusisha wadau wa kilimo, wananchi, wataalamu mbalimbali, wenyeviti kutoka kila Halmashauri pamoja na wakurugenzi.
Mhe. Mbano amewataka wananchi na wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ili iwe chachu ya maendeleo na kuwezesha kufungua fursa za kiuchumi na ajira mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi wa manispaa ya songea, Dkt. Frederick Sagamiko alisema kuwa viongozi, wadau pamoja na wananchi kuendelea kutumia fursa zilizopo za uwekezaji ili kuinua uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Aidha, Mkurugenzi wa Miradi ya Sera na UNDP Amon Manyama amewataka wadau wa kilimo kutumia njia bora na za kisasa ambazo zitawezesha kuongeza ufanisi katika kilimo cha mahindi ya njano ili kuongeza uzalishaji wa mazao bora, ikiwemo na kilimo cha umwagiliaji. Alibainisha
Mwekezaji wa kampuni ya “SMART FOR IMPORT & EXPORT” Mr. Bassem amesema wamekuja Tanzania kwaajili ya kuwekeza katika ununuzi wa mahindi ya njano kuanzia tani milioni moja 1,000,000 kwa mwaka kwa lengo la kupeleka nchini Misri kwa shughuli mbalimbali.
Mr. Bassem ameongeza katika kutekeleza kwa ufanisi, Kampuni ya Import and Eaxport watafanya utaratibu wa kuleta mtaalamu wa kilimo kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali ili kuhakikisha wakulima wanalima kilimo bora na chenye tija.
Hata hivyo wadau wa kilimo wakiongea kwa nyakati tofauti walisema “wako tayari kutoa ushirikiano wa dhati kwa kampuni hiyo ya uwekezaji kwa kusudi la kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
MWISHO.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa