MRADI wa ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambacho serikali imetoa shilingi milioni 400 unatarajia kukamilika mwanzoni mwa mwezi ujao.
Kituo hicho kikikamilika kinatarajia kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 45,000 wanaoishi katika kata za Ruvuma,Subira,Mateka na majengo.
Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mhandisi Karoline Bernad amesema ujenzi unaendelea vizuri ambapo hadi sasa kazi ya kukamlisha inaendelea ambapo majengo matatu kati ya manne yameezekwa na kazi ya kukamilisha inaendelea.
Hata hivyo amesema jengo ambalo bado halijaezekwa hadi sasa ni moja tu ambalo ni jengo la maabara ambalo mafundi wanaendelea kukamilisha.
Kulingana na Mhandisi huyo majengo ambayo yameezekwa katika mradi huo ni wodi ya mama na mtoto,jengo la upasuaji na jengo la huduma kwa watu wa nje na kwamba jengo la maabara ndiyo pekee ambalo bado halijaezekwa…
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa