Na; Amina Pilly.
Kituo cha Afya cha Mjimwema kilichopo katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, kimezindua rasmi huduma mpya ya haraka kwa wagonjwa (Fast Track Service) mnamo Oktoba 01, 2025. Huduma hiyo imelenga kutoa matibabu kwa haraka kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka bila kulazimika kusubiri kwenye foleni ndefu.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi, pamoja na baadhi ya wagonjwa waliopata nafuu. Huduma hii ni ya hiari na itatolewa kupitia jengo maalum litakalokuwa na sehemu muhimu ikiwemo duka la dawa (pharmacy), maabara, vyoo, vyumba vya daktari na eneo la kupumzikia wagonjwa. Kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa, gharama ya kumuona daktari kupitia huduma hii itakuwa shilingi 10,000.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mganga Mfawidhi wa kituo hichoDkt. Alice Kitindi, alisema kuwa huduma hii inalenga kuboresha upatikanaji wa huduma bora na ya haraka kwa wale wanaohitaji huduma za haraka zaidi.

Kwa upande wake Bi. Mariana Masawe, ambaye ni Kaimu Afisa Utumishi na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, alitoa pongezi kwa uongozi wa kituo hicho kwa ubunifu wao wa kuboresha utoaji wa huduma huku akieleza kuwa huduma hiyo itakuwa kichocheo cha ufanisi katika sekta ya afya.
Huduma ya "Fast Track" ni hatua chanya katika kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma stahiki kwa wakati. Huu ni mfano bora wa ubunifu unaojibu mahitaji halisi ya jamii na unapaswa kuigwa na vituo vingine vya afya nchini.
MWISHO.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa