MBUNGE wa Jimbo la Songea mjini Dk.Damas Ndumbaro amewaambia wananchi wa Manispaa ya Songea kuwa kiwanda cha tumbaku kilichopo mjini Songea ambacho kilifungwa kwa muda mrefu kinatarajiwa kuanza kazi mwaka huu àmbapo mafundi toka nchi Italia wamefika kukagua kiwanda hicho mwezi huu na wameamua kuziondoa mashine zote za zamani ili kufunga mashine mpya za kisasa.
Kiwanda hicho kinatarajia kutoa ajira rasmi zaidi ya 2000 na ajira ambazo sio rasmi zaidi ya 5000. Dk.Ndumbaro alikuwa katika ziara ya kutembelea kata zote 21 za Manispaa ya Songea ambayo ilianzia Februari 23 na kukamilika Machi nne mwaka huu
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa