UCHAFUZI wa mto Ruvuma unaofanywa na wachimbaji wa madini katika nchi ya Tanzania na Msumbiji unatishia ustawi wa viumbehai wakiwemo binadamu na viumbehai wa majini na ardhini.
Afisa Maliasili wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wanatumia mito inayomwaga maji yake mto Ruvuma kusafishia dhahabu kwa kutumia kemikali ya zebaki ambayo inaingia moja kwa moja hadi mto Ruvuma.
Kwa mujibu wa matokeo ya maabara kwenye vyanzo vya maji vya Songeapori mkoani Ruvuma vilivyochukuliwa vinaonesha kuwa chanzo hicho ambacho kinamwaga maji yake mto Ruvuma kina kiwango kikubwa cha zebaki ambacho ni 0.02(Hg) ambapo kiwango cha kawaida kinachokubalika ni 0.005(Hg).
Vipimo vya maabara za uchunguzi wa maji vilivyochukuliwa kati ya mwaka 2008 hadi 2010 ,vilibaini kuwa maji hayo pia yana kiwango kikubwa cha taka/tope(turbidity) ambacho kinavuka kiwango kinachokubalika na Shirika la Afya Duniani.zebaki inaweza kusababisha kansa mbalimbali zikiwemo kansa ya tumbo,ini,koo,ngozi na magonjwa mengine.
Imeandikwa na Albano Midelo
Mwanahabari Mwandamizi katika masuala ya mazingira
Mawasiliano albano,Midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa