KILELE cha kumbukizi kinatarajia kuwa Februari 27 mwaka huu ndani ya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea .Hapa ni moja ya vivutio vya utalii wa kishujaa ambapo ni kaburi la pamoja la mashujaa 66 ambao walizikwa humu mara baada ya kunyongwa na wajerumani kipindi cha vita ya Majimaji mwaka 1906.Shughuli rasmi za kuelekea kilele zinaanza kesho Februari 25 na kuendelea mfululizo hadi siku ya kilele.Mkurugenzi wa makumbusho ya Taifa ya Majimaji Mhifadhi Kiongozi Batazar Nyamusya anasema maadhimisho ya mwaka huu yana hadhi ya kimataifa kwa sababu wamealikwa machifu toka nchi mbalimbali ziliwemo Afrika ya kusini,Cameroun,Malawi na Zambia.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa