TAMASHA la kitalii la wilaya ya Nyasa lenye lengo la kuvitangaza vivutio vya utalii na uwekezaji vilivyopo katika wilaya ya Nyasa linatarajia kuanza Januarii Mosi 2019 na kilele chake Januari 6,2019.
Tukiwa tunaelekea katika tamasha hilo hebu tuangalia vivutio adimu vya utalii ambavyo vinaifanya wilaya ya Nyasa kuwa kitovu cha utalii katika ukanda wa kusini.Ziwa Nyasa limebarikiwa kuwa na visiwa vya kuvutia ambavyo vina utajiri wa miti,wanyamapori,wadudu ,samaki na viumbe wengine.Miongoni mwa visiwa hivyo ni visiwa vya Mbambabay(Zambia),Lundo na Puulu ambavyo vinatarajia kufungua milango ya utalii baada ya visiwa hivyo kubainika kuwa na vivutio adimu vya utalii.Kisiwa cha Mbambabay kipo meta 300 toka ufukweni mwa ziwa Nyasa,kisiwa hicho kina utajiri wa aina mbalimbali za samaki wa mapambo ambao ni kivutio cha watalii.Kisiwa Mbambabay kina hekta 27 , kisiwa cha Lundo kina hekta 20 kipo mbali kidogo toka mjini Mbambabay kama unavyokiona nyuma yangu na kisiwa cha Puulu kipo Liuli.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa