SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kukarabati majengo yote ya shule ya sekondari ya Songea Girls iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Shule hii kongwe iliyoanzishwa mwaka 1974 ina wanafunzi 850 wanaosoma kuanzia kidato cha tano na sita.
Afisa Elimu Sekondari Devota Luwungo amesema hadi sasa ni mabweni mawili tu ndiyo yamekarabatiwa kati ya sita na kwamba ukarabati ambao unafanywa na Wakala wa Majengo Tanzania umesimama hali ambayo imesababisha msongamano mkubwa katika mabaweni na kufanya baadhi ya wanafunzi kulala wawili wawili hali ambayo sio salama kiafya na kimaadili.Mkataba wa mradi huu ni wa mwaka mmoja ambao unaanzia Januari 10,2018 na kukamilika Desemba 10,2018 hivyo Mkataba umemalizika wakati idadi ya majengo mengi bado hayajafanyiwa ukarabati na TBA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa