MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA ANAUZA VIWANJA VILIVYOPIMWA KATIKA ENEO LA LILAMBO NA NAMANDITI KWA MATUMIZI YA MAKAZI.
BEI YA VIWANJA HIVYO NI SHILINGI 2000 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA.VIWANJA HIVYO VIPO PEMBEZONI MWA BARABARA YA SONGEA-MBINGA,UMBALI WA KILOMETA 12 KUTOKA KATIKATI YA MJI.
MIUNDOMBINU WEZESHI YAANI MAJI,BARABARA NA UMEME ZIPO KWENYE ENEO LA MRADI.AIDHA BARABARA ZOTE ZA NDANI YA MIRADI ZITACHONGWA NA ZITAPITIKA WAKATI WOTE.
FOMU ZA MAOMBI ZINAPATIKANA KATIKA OFISI YA IDARA YA ARDHI NA MIPANGO MIJI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA KUANZIA SAA 3.00 ASUBUHI HADI SAA 9.00 ALASIRI KUANZIA SIKU YA JUMATATU HADI IJUMAA,BEI YA FOMU NI SHILINGI 20,000 KWA KILA FOMU MOJA NA GHARAMA HIYO HAITARUDISHWA.
PIA WANANCHI WOTE WALIOSHIKILIA VIWANJA VILIVYOPIMWA KATIKA ENEO LA NAMANDITI KWA KULIPA PUNGUFU AU KUTOLIPA KABISA,WANATAKIWA KUMALIZIA MALIPO HAYO MAPEMA.
MKURUGENZI WA MANISPAA ANAKUSUDIA KUVIUZA VIWANJA HIVYO KWA WAOMBAJI WENGINE WATAKAOKUWA TAYARI KUVILIPIA NA KUVIENDELEZA BILA KURUDISHIWA MALIPO YALIYOLIPWA AWALI.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA KUNUNUA VIWANJA VILIVYOPIMWA NA VYENYE HATI.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa