Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Alto Liwolelu katika kikao cha Kamati ya Lishe cha kawaida kilichofanyika tarehe 25/06/2020.
Alto alisema “ Lishe bora maana yake ni kula chakula cha kutosha na chakula kinachofaa ili kiweze kuusaidia mwili kukua vyema, kwa afya njema na kuweza kupigana na magonjwa mwilini. Aliongeza kuwa Utapiamlo ni lishe mbaya na hutokea ikiwa unakula chakula kidogo sana/ kingi sana/ au kula chakula kisichokuwa na lishe ya kutosha.”
Alifafanua kuwa Lengo la Mradi Elimu ya Lishe ni kutoa Elimu ya Lishe kwa Jamii hususani hunyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa muda usiopungua miezi sita ya awali au zaidi, utumiaji wa chakula bora , Kutoa elimu ya Udumavu kwa jamii, kufahamu makundi ya vyakula na mpangilio wa mlo kwa siku.
Naye Mganga Mkuu Manispaa ya Songea Amos Mwenda alifafanua kuwa katika kipindi cha January-March 2020 Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepambana na Udumavu pamoja na Utapiamlo na kufanya uchunguzi wa hali ya Lishe kwa kutumia Mzingo wa Mkono kwa Mtoto chini ya miaka mitano “5” kama ifuatavyo; Waliochunguzwa hali ya lishe ni (18,848), Waliogundulika kuwa na Utapiamlo Mkali ni (15) sawa na 0.1%, Waliogundulika kuwa na Utapiamlo wa Kadiri ni (37) sawa na 0.2%, Wasiokuwa na Utapiamlo (18,796) sawa na 99.7%.
Mwenda, akibainisha baadhi ya Mikakati waliyojiwekea ili kupambana na Utapiamlo na Udumavu Manispaa ya Songea ni pamoja na Kutoa Elimu ya ulishaji wa chakula kwa Watoto Wachanga/ Wadogo kwa kupitia RCH Kliniki pamoja na Watoa huduma CHW, kutoa Elimu kwa akina mama wajawazito mara tu wahudhuriapo kliniki, kutoa Elimu ya uhifadhi salama wa chakula kwa kupitia Vyombo vya Habari, kutoa Elimu ya umuhimu wa kuwa na choo bora, uwekaji wa miundo mbinu ya kunawa mikono na Sabuni nje ya choo, kutibu Maji ya kunywa, pamoja na utoaji wa matone ya Vitamin A kwa watoto. nk.
Aliongeza kuwa pamoja na mikakati waliyojiwekea, Manispaa ya Songea inaendelea kutoa elimu ya uzalishaji bora wa mazao ya chakula, mifugo na uvuvi, Kilimo cha mboga mboga, kwa kupitia vikundi vya wanawake, Vijana, na Walemavu ili waweze kukopa mikopo yenye riba nafuu inayoendelea kutolewa na Serikali kupitia Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo kukuza mitaji yao na kujipatia kipato katika familia. Alisema Kwasasa Mikopo hiyo inaendelea kutolewa kwa kupitia vikundi vya Wanawake 4%, Vijana 4%, na Walemavu 2% sawa na 10% ambayo ni makusanyo ya mapato ya ndani ya kila mwezi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI- MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa