Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa saba inayozalisha mazao ya chakula na biashara kwa wingi nchini Tanzania, ambapo kwa mwaka 2019 Mkoa wa Ruvuma uliongoza kwa mazao mengi ya chakula kwa nchi nzima.
Hayo yamebainika katika uzinduzi wa maadhimisho ya maonesho ya nanenane yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Nanenane mjini songea jana 04/08/2020.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Ishenye.
Ishenye alisema Mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2015 ulikuwa na jumla ya ng’ombe 117,334, mbuzi 227,186, kondoo 22,432, na nguruwe 223,676, ambapo kwa mwaka 2020 mifugo hii imeongezeka na kufanya Mkoa kuwa na Ng’ombe 190,514, Mbuzi 272,147, Kondoo 30625, Nguruwe 315,923, ambapo ongezeko hilo la mifugo limepelekea uzalishaji wa mifugo kuongezeka na kufikia tan 7851 za nyama ya ng’ombe, tan 4906 za nyama ya Mbuzi, tan 871 za nyama ya Kondoo, na tan 14,033 za nyama ya Nguruwe, wakati huo uzalishaji wa mayai umeongezeka na kufikia mayai mil 112,418,647 hadi mwezi may 2020.
Aliongeza kuwa “ Mh. Rais Dr John Pombe Magufuli ametoa fedha Tsh Bilioni 3 (tatu) kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya kisasa iliyopo kata ya Tanga Manispaa ya Songea yenye uwezo wa kuchinja Ng’ombe 100 na Mbuzi 200 kwa siku ambayo ni hazina kwa wachinjaji na Wananchi kwa ujumla.”
Kauli mbiu katika maadhimisho ya Nanenane 2020 ; Kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi chagua viongozi bora 2020.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY,
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
05.08.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa