Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Ahmed Abbas Ahmed ameongoza wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika kuadhimisha maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanzania ambayo huadhimishewa kila mwaka ifikapo tarehe 26 Aprili ambapo kwa Mkoa wa Ruvuma maadhimisho hayo yamefanyika Manispaa ya Songea kwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Zimamoto Songea.
Sambamba na mazoezi hayo tarehe 25 April iilifanyika mkesha katika uwanja wa Matarawe ulioshirikisha wananchi kwa lengo la kusikiliza Hotuba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na wananchi uwanjani hapo alisema" amewataka wananchi kuuenzi muungano wetu ambao ulianzishwa na viongozi wetu." pia amewataka wanancha kufanya mazoezi kila jumamosi ya pili ya mwanzo wa mezi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa