MAFUNZO ya siku nne ya tovuti yenye lengo la kuimarisha mifumo ya sekta ya umma yameanza wiki hii yakiwashirikisha maafisa habari na TEHAMA toka mikoa ya Ruvuma,Lindi,Mtwara na Dar essalaam .Mafunzo hayo ambayo yanamalizika Aprili 13 yanafanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mtwara.Mafunzo haya yanatarajia kuongeza mwelekeo kwa mifumo ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa Tanzania kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Mada mbalimbali zimetolewa na wawezeshaji Budodi Rodiney,,Atley Kuni na Faith Shimba na kwamba ili kuhakiisha maafisa habari na TEHAMA wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa kwa mara ya kwanza kitini cha mafunzo ya uandishi wa Tovuti kimetolewa kwa sekretarieti za mikoa na Mmlaka za serikali za mitaa.Kitini kimetaraishwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Hbari na Michezo,Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) na mradi wa Iumarishaji Mifumo ya Sekta za Umma(PS3) unaofadhiliwa na Shirikalla Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa