• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MAAFISA kilimo Nyasa wapewa mafunzo ya kuboresha kilimo cha kahawa

Tarehe ya kuwekwa: December 6th, 2019

Viongozi wa vyama tisa(9) vya  Ushirika vya Msingi vya mazao (AMCOS ) katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga wamepatiwa mafunzo ya kukuza njia asilia za kilimo ili kuwa saidia wakulima kuongeza ubora na kuhakikisha kunakuwa na kuhakikisha kunakuwa na kahawa bora kwa sasa na kwa baadaye kwa mtumiaji yeyote.

Mafunzo hayo yamefanyika  leo katika Ukumbi wa WALIOCHONACHO NA WASIOKUWANACHO uliopo Mtaa wa Ruhuwiko Mjini Mbinga yaliyotolewa na Kampuni ya Kahawa ya Starbucks yenye makao yake makuu jijini Mbeya na lengo lamafunzo hayo ni kukuza njia asilia za kilimo cha kahawa, ili kuwasaidia wakulima kuboresha zao la kahawa, na kuongeza ubora na kuhakisha kunakuwa na kahawa bora kwa sasa na kwa baadaye

 akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa Idara ya kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Bw.Menance Ndomba alisema Halmashauri ya Wilaya ya Nyasaitawachukulia hatua kali maafisa kilimo wote ambao hawatawasaidia wakulima kuongeza ubora wa kahawa ili kuwapa maendeleo wananchi.  

Bw. Ndomba amefafanua kuwa atahakikisha Maafisa kilimo wote Wilayani Nyasa, ambao watashindwa kuwapa elimu wakulima ili wazalishe kahawa yenye ubora atahakikisha anawachukulia hatua za kinidhamu pamoja na kuwafukuza kazi.

Aliongeza kuwa kahawa ni zao la kimkakati ambalo Serikali imelipa kipaumbele hivyo maafisa kilimo wanatakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuwapa elimu wakulima na kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuzalisha kahawa yenye ubora na nyingi na kupelekea wananchi  wanapata maendeleo.

“Maafisa kilimo wa Wilaya ya Nyasa nitawapima kwa kuangalia wananchi wamepata ubora gani wa kahawa. Afisa kilimo mmeajiriwa kwa kazi ya kuhakikisha wananchi/wakulima wanakuwa na maendeleo kwa kuzalisha mazao yenye ubora na yakutosha.Tunapozungumzia maendeleo ni pamoja na kuhakikisha Wakulima wanakuwa na elimu ndelevu ya mazao mbalimbali hasa mazao ya kimkakati. Nichukue fursa hii kuwaambia Nyasa hatumtaki Afisa kilimo asiyetoa elimu kwa wakulima wake ili waweze kuzalisha mazao bora.

Aidha bw.Ndomba ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha na kusimamia mfumo wa Vyama vya Msingi vya Ushirika vya Mazao (AMCOS) kwa kuwa wakulima wameweza kuuza kahawa zao kwa pamoja kwa bei mzuri, kuweza kufanya manunuzi ya Pembejeo kwa pamoja (Bulk purchase)  hususani mbolea ambapo AMCOS zilizopo Nyasa tayari zimeshanunua mbolea na kusambaza kwa wanachama wake.

Naye Meneja wa Kampuni ya Stabucks Farmers Center amesema kahawa inayotoka Wilaya ya Mbinga na Nyasa ni nzuri na inapendwa katika soko la Dunia kwa kuwa ni ya asili, hivyo tunatakiwa  kuongeza ubora wa kahawa yetu na kuulinda ili bei iwe nzuri, mkulima anufaike zaidi kwa kuuza bei ya juu kwa kuwa ubora wa kahawa unaongeza Bei katika soko la Dunia.

Aliwapongeza wakulima hao kwa kazi nzuri ya kuzalisha kahawa nzuri, na kuwataka kuongeza uzalishaji wa kahawa inayolimwa katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga.

Mafunzo haya ni ya siku moja yaliyowakutanisha Viongozi wa vyama vya msingi vya wakulima wa kahawa, Maafisa kilimo na wadau wa zao la kahawa.

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa