VITABU vitakatifu vimeandika kuwa Mwenyezi Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana,inaaminika kuwa vitu visivyoonekana ni vingi kuliko vinavyoonekana.
Viumbe hao wa ajabu waishio angani wanaitwa Aliens.Inaaminika wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizopita wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).
Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.Inaaminika kuwa Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknojia kuliko binadamu tatizo tuu hawavai nguo!!
Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.
Haijulikani moja kwa moja viumbe hawa wa ajabu wanaishi sayari gani lakini Pia inaaminika waliwahi kuonekana Kisiwa cha Bermuda pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida, Marekani.
Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe hao.Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana milele ,inaaminika viumbe Aliens ndiyo wahusika wa upotevu huo.Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani tangu enzi hizo kabla ya binadamu na hawajaondoka.
Inaaminika viumbe hawa wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.Wataalam wa anga wanadai kuwa kazi ambazo zinafanywa na Aliens kwa siku moja binadamu anaweza kutumia miaka 100 kufanyakazi hiyo kwa hiyo viumbe hao wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka.
Imeandaliwa na Albano Midelo kwa msaada wa mitandao ya kihabari
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa