KAMPUNI ya kimataifa ya serikali ya China inayoitwa China Sichuan International Co-operation (SIETCO) imeanza rasmi maandalizi ya ukarabati wa barabara za Manispaa ya Songea kwa kiwango cha lami nzito.
Ukarabati wa barabara hizo zenye urefu wa kilometa 10.3,unatarajia kukamilika Septemba 30,2019.Mkataba ni wa miezi 18,fedha ambazo zinatumika katika ukarabati huo ni bilioni 10.96,Mkandarasi wa sasa anaongeza kilometa zaidi ya mbili,pia ataweka taa za barabarani.
Barabara za Manispaa ya Songea ambazo zipo kwenye mradi huu ni FFU hadi Matogoro yenye urefu wa kilometa 3.2,barabara ya Songea Girl’s hadi Mateka yenye urefu wa kilometa 1.5 na barabara ya Mwembechai hadi Bombambili yenye urefu wa kilometa 2.6.
Barabara nyingine ni Mitumbani hadi Yapenda yenye urefu wa kilometa moja,barabara ya Polisi hadi Stendi ya Mlilayoyo yenye urefu wa kilometa 0.45.
Imetolewa na Albano Midelo
Mei 7,2018
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa