MRADI wa machinjio ya kisasa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi zaidi ya bilioni tatu upo mbioni kukamilika na kukabidhiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Mradi huo unaojengwa katika kata ya Tanga Manispaa ya Songea hadi sasa unakaribia asilimia 100 ya ujenzi ambapo Mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo Kampuni ya Giraffe ameahidi kukamilisha mradi huo wakati wowote kuanzia sasa.
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Songea,tayari imekagua mradi na kumuagiza Mkandarasi kukamilisha kazi hiyo haraka.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa