MADIWANI WA SONGEA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO MOROGORO
KUNDI la kwanza la waheshimiwa Madiwani 13 na watalaam watano wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma limefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Madiwani hao wakiwa na wenyeji wao,waheshimiwa madiwani wa Manispaa ya Songea wamejifunza kuhusu ukusanyaji mapato, usimamizi wa taka na masuala ya mazingira kwa ujumla.
Kundi la pili la waheshimiwa Madiwani 15 na watalaam saba linatarajia kufanya ziara ya mafunzo kama hayo katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuanzia Juni 5 hadi 9 mwaka huu.
Ziara hizo za mafunzo toka katika Manispaa hizo mbili ambazo zimefanikiwa katika ukusanyaji mapato na suala zima la usafi wa mazingira, zinatarajia kuboresha suala la ukusanyaji wa mapato na suala zima la mazingira katika Manispaa ya Songea.
Katika suala zima la usafi wa mazingira,Manispaa ya Songea inazalisha taka kiasi cha tani 71.5 kwa siku ambapo uwezo wa Manispaa hiyo kuzoa taka kwa siku ni kati ya tani 35 hadi 40 hali inayosababisha tani 31.5 kubaki bila kuzolewa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa