TASAF imeendesha na zoezi la utoaji wa mafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani kwa lengo la kutambulisha utekelezaji wa mradi wa TASAF awamu ya pili iliyofanyika katika ukumbi wa SACCOS ya Walimu ambayo ilihudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Akizungumza Mkurugenzi Uratibu TASAF Bi Haika Mavika alisema Mradi huo ni Mpango uliolenga kuwasaidia watu wenye kipato cha chini (masikini) ili waweze kujikwamua kutoka katika kiwango cha chini na kwenda hatua nyingine.
Bi Haika aliongeza kuwa, Kwa mwaka 2022 Manispaa ya Songea ilikuwa na miradi 84 yenye thamani ya zidi ya Bil 1 ambayo baadhi yake imekamilika ambapo aliwataka viongozi hao kutembelea miradi ya TASAF kwani ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya Halmashauri.
Kwa upande wa Naibu Meya alitoa shukrani kwa Serikali kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatawezesha kufahamu namna ya kusimamia miradi ya TASAF .
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa