Kwa mujibu wa kanuni ya 9 ya kanuni ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa kamati ya Mtaa katika mamlaka za Miji za mwaka 2024, Msimamizi wa Uchaguzi amepewa mamlaka ya kutoa maelekezo kuhusu uchaguzi.
Tamko hilo limetolewa tarehe 26 septemba 2024 na Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Songea Wakili. Bashir Muhoja akiwa kwenye kikao cha kutoa maelekezo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kuhakikisha taratibu zote zinafuata kwa wapiga kura na wagombea.
Maelekezo yaliyotolewa ni pamoja na tarehe ya uchaguzi, muda na Sehemu ya kuandikisha wapiga kura, muda na mahali pa kufanyia uchaguzi, Wito kwa wakazi wenye sifa za kupiga kura, Wito wa kwa wagombea, kuchukua na kurudisha fomu, uteuzi wa wagombea, pingamizi dhidi ya uteuzi, Rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi la uteuzi, na kampeni za uchaguzi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa, wataalamu, pamoja watendaji wa kata.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa